MKUTANO MKUU WA TATU WA BARAZA LA TAIFA LA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA (NACOPHA) WAMALIZIKA.

uploaded 22/11/2018

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Mkutano Mkuu wa tatu wa Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na VVU ulianza mnamo tarehe 15 Novemba 2018 nakumalizika tarehe 16 Novemba 2018, katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma. Mkutano huo ulifunguliwa na katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, ajira, vijana, na watu wenye ulemavu Prof. Faustin Kamuzora aliyemuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa.


Serikali imewaahidi watu wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI nchini kutofumbia macho changamoto wanazokabiliana nazo na kuhakikisha inaendelea kuboresha huduma za UKIMWI hapa nchini hayo yalisemwa kupitia hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa iliyosomwa kwa niaba yake na Prof. Faustin Kamuzora 
Amesema kupitia hotuba ya mwenyekiti wa NACOPHA bwana justine Mwinuka alibaini changamoto

mbalimbali zinazowakabili WAVIU ambazo ni pamoja na umbali wa vituo vya matibabu na kutumia muda mrefu kwenye vituo vya matibabu,kipato duni cha WAVIU kugharamia matibabu,lugha na vitendo vya unyanyapaa katika vituo vya kutolea huduma, uhaba wa mashine za kupimia wingi wa Virusi kwenye damu na kuratibu wadau wote kwa Ushirikishwaji wa WAVIU kwenye mwitikio wa UKIMWI kupitia muundo wa konga za WAVIU.


Aidha amesema katika kukabiliana na changamoto hizi, serikali imeendelea kufanya juhudi za kuzipunguza na hata kuzimaliza kabisa kwa kuongeza idadi ya vituo vya afya vinavyotoa huduma ya matibabu ya VVU “hadi kufikia July 2018 tuna vituo visivyopungua 8000 vya kutolea huduma za matibabu ya VVU, pia tumeweza kusajiri WAVIU 839,544 kufikia mwishoni mwa mwaka 2017”


Mkutano huu umeenda sambamba na Baraza kutambua na kutunukia nishani za heshima kwa baadhi ya Viongozi kwa kutambua michango yao mikubwa katika mwitikio wa UKIMWI. Waliotunukiwa nishani hizo ni pamoja na Mhe, Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa, Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, Mkurugenzi mstaafu wa TACAIDS Bi. Fatuma Mrisho, Mwenyekiti mstaafu wa NACOPHA bwana Vitalis Makayula na Mwenyekiti wa NYP+ Nevala Kyando.

Prof. Faustin Kamuzora akikabidhiwa nishani ya heshima kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Majaliwa Kassim Majaliwa na Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi awamu ya Pili bw. Justine Mwinuka.

 

Mhe Oscar Mukasa Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI akipokea nishani ya heshima kwa niaba ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai

Mkurugenzi mstaafu wa TACAIDS Bi. Fatuma Mrisho akipokea nishani  ya heshima kutoka kwa aliyekuwa mwenyekiti wa Baraza bw. Justine Mwinuka.

 Mwenyekiti mstaafu wa NACOPHA bwana Vitalis Makayula Mwenyekiti wa Kwanza wa Baraza akipokea nishani ya heshima kutoka kwa mwenyekiti wa awamu ya pili bw. Justine Mwinuka

 Mwenyekiti wa NYP+ Nevala Kyando akikabidhiwa nishani ya heshima kutoka kwa mwenyekiti  wa Baraza wa awamu ya pili ndugu Justine Mwinuka

Pamoja na hayo Mkutano Mkuu uliweza kuwachagua viongozi Bodi ya Baraza la Taifa la WAVIU ambapo wafuatao walichaguliwa kuwa viongozi wa bodi kwa nafasi ya Mwenyekiti ilitwaliwa na Bi Leticia Mourice Kapela wa konga ya Bukombe, Makamu Mwenyekiti bwana Yusufu Alfred Merere mweka hazina Mitterrand Mohamed Dagila na wajumbe Shamila Ibrahim, Elias Charles, Christina Martin, Deogratius Clevass, Francis Stolla, Hermes Mutagwaba, Pudensiana Mbwiliza na Amir Mahamud.


Msimamizi wa Uchaguzi akionesha vifaa vilivyotumika kuwekea kura za wagombea zikiwa tupu kabla ya uchaguzi kuanza

 

Wajumbe wa Mkutano wakipiga kula kuchagua viongozi wao

Mbali na uchaguzi wa bodi walichaguliwa pia wawakilishi wa WAVIU kwenye TNCM ambao ni Japhes Baitani na Pudensiana Mbwiliza 


Mkutano mkuu wa NACOPHA hufanyika kila baada ya miaka mitatu kwa kuwakutanisha wawakilishi kutoka Tanzania Bara na wadau wengine wa UKIMWI ukiwa na lengo la kutathimini utekelezaji wa Baraza kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kupata taarifa ya mwelekeo wa Baraza kwa kipindi kinachofuata na kujadiliana kuhusu mafanikio na changamoto zinazowapata WAVIU kote nchini pamoja na utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa kufikia tisini tatu (90-90-90) .

#nacophamk2018

  • COAT OF ARM
  • UNAIDS
  • USAID
  • TACAIDS
  • GLOBAL FUND
  • GNP


The National Council of People Living with HIV & AIDS in Tanzania (NACOPHA) Mbezi Beach Area, Block 'F' Plot no. 450/5 Mwai Kibaki Road, Kinondoni District, Dar es Salaam,Tanzania
Copyright © 2019 NATIONAL COUNCIL OF PEOPLE LIVING WITH HIV TANZANIA