NACOPHA inaungana na wanawake wote Tanzania katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yenye kaulimbiu “50 – 50 ifikapo 2030; Tuongeze Jitihada”

uploaded 08/03/2016

Kila tarehe 8 machi ya kila mwaka Tanzania huungana na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha siku ya wanawake Duniani.

Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) linaungana na Wanawake wote Tanzania na Dunia kwa ujumla katika kuadhimisha siku hii muhimu ya Wanawake duniani ili kuendeleza Utetezi wa Haki za wanawake na Usawa wa kijinsia, ifikapo 2030 kuwe na asilimia 50 kwa 50 ya ushiriki wa wanawake na wasichana katika Nyanja zote za maendeleo.

Katika Kufikia Malengo hayo NACOPHA inatoa wito kwa Wanawake wote Tanzania Kuongeza Jitihada siyo tu katika katika kufikia malengo ya 50 kwa 50 ifikapo 2030 bali pia kufikia malengo yaliyowekwa kimataifa 90% 90% 90% ya Mkakati wa Kupunguza maambukizi ya VVU ifikapo 2020 yaani:-

90% kwa waliopima afya zao na kutambua hali yao ya maambukizi,

90% wanaostahili kupatiwa tiba wanapata tiba na kubakia katika tiba na

 90% ya waliopo kwenye tiba wawe na kiwango kidogo cha virusi kwenye damu

  Lengo likiwa ni kufuta kabisa UKIMWI ifikapo mwaka 2030.

Rai yetu kwa Wanawake wote: sasa ni wakati muafaka kujitokeza kwa wingi katika mwitikio wa UKIMWI ili kudhibiti ongezeko la maambukizo ya VVU na kuhakikisha tunafikia sifuri tatu ifikapo mwaka 2030.

 

Tunawatakia Mafanikio mema katika kuadhimisha siku ya Wanawake duniani.

  • COAT OF ARM
  • UNAIDS
  • USAID
  • TACAIDS
  • GLOBAL FUND
  • GNP


The National Council of People Living with HIV & AIDS in Tanzania (NACOPHA) Mbezi Beach Area, Block 'F' Plot no. 450/5 Mwai Kibaki Road, Kinondoni District, Dar es Salaam,Tanzania
Copyright © 2019 NATIONAL COUNCIL OF PEOPLE LIVING WITH HIV TANZANIA