Jamii yatahadharishwa UKIMWI upo

uploaded 09/06/2016

BARAZA la Taifa la watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania (NACOPHA) limeitahadharisha jamii kujilinda dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na kuondokana na fikra kwamba ugonjwa huo umeisha, kwani bado ni tishio.

Hayo yamezungumzwa na Meneja Ufuatiliaji wa Tathimini wa NACOPHA, Rachel Jacob wakati wa mafunzo ya watoa huduma ngazi ya jamii, vituo vya afya na maofisa ustawi wa jamii yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

“Jamii inapaswa kuchukua taadhari kwani maambukizi bado yapo hivyo tunapaswa kubadilika na kuwa na tabia ya kupima VVU (Virusi vya Ukimwi) mara kwa mara ili kujua afya zetu,” alisema.

Alisema kuwa Nacopha wameanzisha mradi wa ‘Sauti yetu’ ambao unawahusisha watu wanaoishi na VVU ili kusambaza elimu kwa jamii, kukabiliana pamoja na kujikinga na maambukizi hayo.

Kwa upande wa Daktari wa Kituo cha Afya cha Pungu Kajiungeni, Honest Lyimo alisema hali ya maambukizi bado ipo juu huku wanandoa wengi wakiwa hatarini.

 

“Nilifanya utafiti katika kituo chetu, na kugundua kuwa wanandoa wengi siyo waaminifu na wamekuwa wazito kutumia kinga hata pale wanapotoka nje ya ndoa huku wengi wanakutwa na maambukizi zaidi ya vijana walio nje ya ndoa,” alisema

  • COAT OF ARM
  • UNAIDS
  • USAID
  • TACAIDS
  • GLOBAL FUND
  • GNP


The National Council of People Living with HIV & AIDS in Tanzania (NACOPHA) Mbezi Beach Area, Block 'F' Plot no. 450/5 Mwai Kibaki Road, Kinondoni District, Dar es Salaam,Tanzania
Copyright © 2019 NATIONAL COUNCIL OF PEOPLE LIVING WITH HIV TANZANIA