Hotuba ya Mgeni Rasmi Mratibu wa TACAIDS wa mkoa wa Mwanza, katika ufunguzi wa warsha shirikishi ya siku mbili kwa ajili ya utambulisho na kuandaa mpango wa utekelezaji wa mradi wa SAUTI YETU

uploaded 26/07/2016

HOTUBA YA MGENI RASMI MRATIBU WA TACAIDS WA  MKOA WA MWANZA, KATIKA UFUNGUZI WA WARSHA SHIRIKISHI YA  SIKU MBILI KWA AJILI YA UTAMBULISHO NA KUANDAA MPANGO WA UTEKELEZAJI WA MRADI WA SAUTI YETU  KWA WASHIRIKI WOTE KANDA YA MWANZA MONARCH HOTELI- MWANZA TAREHE 13/04/2016

 

 

 

 

 

 

Ndugu Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na VVU Tanzania

Ndugu Wenyeviti na Makatibu wa Konga zote Mliohudhuria hapa leo

Ndugu Afisa Mtendaji wa Baraza,

Ndugu Watendaji wa Baraza,

Ndugu Wageni waalikwa,

Ndugu Waandishi wa Habari,

Mabibi na Mabwana,

 

Habarini za asubuhi,

Nina furaha kubwa kuungana nanyi siku hii ya leo katika warsha hii muhimu, sio kwenu tu mliohudhuria, bali hata kwa tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI na Taifa kwa ujumla.

 

Nadiriki kutamka kuwa warsha hii  ni muhimu kwa sababu nina imani kubwa kwamba mara tu  mtakapomaliza shughuli hii, kwa siku mbili  mtakuwa chachu ya mapambano dhidi ya UKIMWI katika halmashauri zetu.

 

Ndugu Mwenyekiti wa Baraza

Kwa upande wa Sera ya Taifa ya UKIMWI,imeainisha misingi kadhaa

ikiwemo wajibu na jukumu kwa  jamii  yetu watanzania, na mtu mmoja mmoja  kwa nafasi yake kuhakikisha kuwa wanazuia na

kudhibiti  maambukizi ya  UKIMWI.Kadhalika, jambo jingine muhimu miongoni mwa mambo mengi yaliyoainishwa ni la elimu na mawasiliano kwa jamii. Kwa misingi ya haya yote niliyobainisha, natumaini kuwepo kwenu hapa na haya mliyopanga kuyatekeleza ni mwitikio dhahiri wa kutekeleza kwa dhati maelekezo hayo ya sera na kuleta

 

Ndugu Mwenyekiti wa Baraza

Kwa niaba ya serikali yetu, napenda  kutoa shukrani za dhati kwa wadau wa mbali mbali wa maendeleo , na hasa serikali ya Marekani kwa kuwezesha juhudi za WAVIU kupata fursa ya kutekeleza mradi huu. Ahsanteni sana.  Nimedokezwa kuwa mradi huu umelenga kutoa fursa kwa WAVIU kushiriki moja  kwa moja katika utekelezaji wa Huduma za UKMWI kwenye jamii na kuhakikisha watu wnegi wanakwenda kupima  na kutabua hali zao za maabukizi ya VVU, kuhaklikisha asilimia 90  ya walioambukizwa na VVU wanaanzishiwa na kudumu katika tiba, na pia kuhakikisha waliodumu kweney tiba , asilimia 90 wanakuwa na mfubao wa VVU kwenye damu.  mafanikio ya malengio haya , kwa kiasi kikubwa yanategeme juhudi na ushiriki na ushirikishwaji makini wa WAVIU katika kutoa huduma kwa wale wanaoishi na VVU.  Nimeelezwa luwa mradi huu utatekelezwa katika halmashauri 46 hapa nchni , nanyi ni sehemu ya halmashauri hizo, tafadhalini shiriki kwa ukamilifu na uaminifu kwa majukumu tutakayo pewa,

Kupitia Mradi wa SAUTI YETU, sina budi kuwapongezeni nyote  hapa, kwani  ni dhahiri kuwa  bila juhudi hizi zinazoendelea kufanywa na WAVIU kwa sasa  ndani ya jamii,  UKIMWI unaweza kuleta athari kubwa sana katika sehemu zetu za kazi na kwa uchumi wa nchi yetu kwa ujumla. Naamini kupitia mradi huu na elimu itakayopatikana ndani ya siku mbili hizi, itamfanya kila mmoja wetu kupata uelewa wa dhamira ya mradi wa SAUTI YETU na kuhamasika katika muitikio wa UKIMWI.  

 

Ndugu Wanasemina

Nimefahamishwa hapa kwamba katika siku mbili hizi mtajifunza mambo mbalimbali yakiwemo kuufahamau kwa undani mradi wa SAUTI YETU ikiwemo walengwa, watekelezaji, namna ya utekelezaji, matokeo na kubwa Zaidi na muhimu ni michango yenu juu ya namna gani mradi huu utatekelezwa kwa mafanikio makubwa ndani ya halmashauri za wilaya zetu  . Wito wangu kwenu ni kuwa mradi huu uwe chachu ya mapambano dhidi ya   UKIMWI katika halmashauri zetu , naamini endapo tutatekeleza vyema mradi huu basi hapatakuwa tena na maambukizo mapya katika jamii zetu, tutaongeza idadi ya watu waliopima na kutambua hali zao za maambukizi ya VVU, kuwa na idadi kubwa ya watu waliojua hali zao na kuanza tiba na kuendelea kubakia katika tiba na mwisho tutaweza kuboresha afya na kupunguza uwingi wa virusi ndani ya miili yetu. Ningetamani hili lingeweza kuwekwa kama lengo la kila mmoja wenu aliyepata bahati ya kuhudhuria mkutano huu.

 

Ndugu Mwenyekiti na wanasemina,

Haya yote tunayoyaongelea hapa yanawezekana endapo tutakuwa na dhamira thabiti. Kinachotakiwa ni utekelezaji kwa vitendo wa kila mkakati tutakaojiwekea. Hivyo, Ndugu Mwenyekiti napenda kukuhimiza uendelee kuhakikisha kuwa utekelezaji wa mradi huu unafikia walengwa na kunufaisha jamii nzima ya watanzania

 

Ndugu Wanasemina, Ndugu Wana habari, Mabibi na Mabwana,

Mwisho naomba nimalizie kwa kuwatakia mafanikio  mema  katika malengo mliyojiwekea katika warsha hii mkutano mwema na vile vile kutamka kwamba warsha hii shirikishi  kwa ajili ya utambulisho na kuweka mpango wa utekelezaji wa Mradi

wa SAUTI YETU na mipango juu ya utekelezaji wake sasa umefunguliwa rasmi.

 

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza

  • COAT OF ARM
  • UNAIDS
  • USAID
  • TACAIDS
  • GLOBAL FUND
  • GNP


The National Council of People Living with HIV & AIDS in Tanzania (NACOPHA) Mbezi Beach Area, Block 'F' Plot no. 450/5 Mwai Kibaki Road, Kinondoni District, Dar es Salaam,Tanzania
Copyright © 2019 NATIONAL COUNCIL OF PEOPLE LIVING WITH HIV TANZANIA