Search
Close this search box.

Maadhimisho ya Siku ya Kupinga Unyanyapaa Duniani 2024 (Zero Discrimination Day)

Maadhimisho ya Kupinga Unyanyapaa Duniani yamefanyika mwezi Machi kama hatua ya kutafakari vitendo vya unyanyapaa na ubaguzi katika jamii na kuunga mkono jitihada za kuleta usawa ili kutokomeza VVU. Maadhimisho haya ni moja ya hatua za kuhimiza utekelezaji wa afua za UKIMWI na hususani kinga ya VVU na upimaji VVU.

Kupitia Maadhimisho Haya, Jamii Inapaswa Kufahamu Kuwa:

  1. Unyanyapaa umepungua kutoka 28% mwaka 2006 hadi 5.5% mwaka 2021.
  2. Viongozi wa dini wasaidie kuhimiza jamii kuacha unyanyapaa kwa WAVIU na kuhimiza matumizi ya huduma za VVU na UKIMWI kwa wale wanaotambua hali zao.
  3. Unyanyapaa unachangia kwa kiasi kikubwa mwitikio hafifu wa jamii kukubali kupima VVU na/au kutumia dawa za kufubaza VVU.
  4. Konga za WAVIU ni jukwaa sahihi kwa WAVIU kujumuika na kupeana uzoefu wa matumizi ya huduma za tiba na matunzo kirafiki.
  5. Watu wenye ulemavu wanapaswa kujumuishwa katika utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI kama vile elimu chapishi kwa nukta nundu, wakarimani pale CTC nk.
  6. Kuachana na lugha zinazowabagua na kuwanyanyapaa watu wanaoishi na VVU kama vile kuwaita “waathirika” nk.

Kauli Mbiu ya Mwaka Huu

Kauli mbiu ya mwaka huu inasema “Tulinde Afya Zetu, Kwa Kulinda Haki Zetu” ikiwa na dhamira ya kuangazia kukosekana kwa usawa katika huduma za VVU na UKIMWI na vitendo vya unyanyapaa na ubaguzi.

Msaada na Uungaji Mkono

Mkurugenzi Mkazi wa UNAIDS Dkt. Martin Odiit amesema kuwa shirika lake bado linaunga mkono juhudi za kupinga unyanyapaa na ubaguzi kama hatua ya kuhimiza kufikiwa kwa 95-95-95 ifikapo 2030 nchini Tanzania.

Historia ya Maadhimisho

Yapata miaka 20 sasa toka kuanzishwa kwa maadhimisho haya duniani. Nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania zimeunga mkono maadhimisho haya kila tarehe 1 ya mwezi Machi.

Picha za Tukio

Share the Post:

Get Involved

Make a Difference with NACOPHA

Your support helps us achieve our goals. Whether you volunteer your time, donate resources, or partner with us, your involvement makes a significant impact in the lives of people living with HIV/AIDS in Tanzania.

  • Join us in the fight againt HIV.
  • Let’s work together to provide support for those in need.
  • Donate to our cause